Saturday, June 20, 2020

NATTA SECONDARY SCHOOL JOINING INSTRUCTION FOR JULY 2020


Click here 👇 to Download Joining Instruction


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS – TAMISEMI

SHULE YA SEKONDARI NATTA, S.L.P 192, MUGUMU-SERENGETI

Kumb. Na: KSS/F. V/VOL.I/ 10
Namba za Simu:                                                                 
Mkuu wa Shule: 0752- 985030 au 0787- 985030          
M/Mkuu wa shule:0753 – 741530
Mwandamizi taaluma: 0686 - 777374
Mtatron: 0755 - 057448
Tarehe:  30 /05/2020




************************************************************************************************

Mzazi/Mlezi wa Mwanafunzi........................................................S.L.P..........


YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI NATTA; HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI
MKOA WA MARA MWAKA 2020.
Utangulizi:
Ninafurahi kukutaarifu kuwa mwanao------------------------------------------amechaguliwa  kujiunga na masomo ya kidato cha tano tahasusi ya..................... katika shule ya sekondari ya NATTA. Muhula wa masomo utaanza……………. Hivyo mwanao anatakiwa kuripoti shuleni tarehe……………… kwa usajili na masomo yataanza rasmi tarehe ………. Mwisho wa kuripoti ni   tarehe ………………….  
Mahali shule ilipo
Shule ya sekondari ya Natta ipo Mkoa wa Mara; Wilaya ya Serengeti; Tarafa ya Grumeti; Kata ya Natta umbali wa kilometa arobaini (40) kutoka makao makuu ya wilaya (Mugumu). Usafiri wa barabara ni wa uhakika muda wote.
Jinsi ya kufika Shuleni
(i)             Wanaotoka Dar-Es-Salaam, Pwani; Morogoro; Mikoa ya Kati; Kusini; Nyanda za juu kusini; Kigoma; Kagera baada ya kufika Mwanza wanashauriwa kupanda Mabasi Stendi ya Buzuruga-Mwanza yanayokuja Mugumu kupitia Bunda. Nauli kutoka Mwanza ni kati ya Tsh. 15,000/= hadi 20,000/=.
(ii)            Kwa wale wanaotokea Mikoa ya Kaskazini (Kilimanjaro; Arusha; Manyara na Tanga) wapande mabasi yanayokwenda Musoma kupitia barabara ya Ngorongoro-Serengeti. Nauli kutoka arusha mjini ni Tsh. 45,000/=
(iii)          Kwa wanaotoka Mkoa wa Mara wanaweza kupandia stendi kuu za mabasi yatokayo Musoma, Bunda; au Tarime kuja Mugumu Kupitia Butiama; Nyamswa; Isenye na Kushukia Natta Sekondari. Nauli ni ati ya Tsh. 10,000/= hadi 15,000/= kufika shuleni.
* Mwanafunzi anashauriwa kumuomba mhudumu wa gari (Dereva au Condactor) 
   alilopanda kumshushia KIBAO CHA SHULE YA SEKONDARI NATTA.
2.0. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.
2.1 Ada na Michango ya Shule:
     (a) Ada ya shule kwa  mwaka ni Tsh. 70,000/=. Unaweza kulipa Tsh. 35,000/=
          kwa muhula au kulipa ada yote kwa mara moja.
         Fedha hiyo ya ada ilipwe kenye Akaunti ya Shule Na. 30201200045
         ilitwayo NATTA SECONDARY SCHOOL katika Benki ya NMB Tawi lolote
         na lete Bank Pay in Slip Original shuleni iliyoandikwa Jina sahihi la   
         Mwanafunzi.

(b) Michango inayotakiwa kulipwa na kila mzazi ni:-
      (i)       Tsh. 20,000/= kwa ajili ya ukarabati wa samani
      (ii)      Tsh.   6,000/= kwa ajili ya kitambulisho na picha
(iv)          Tsh. 20,000/= kwa ajili ya taaluma
(v)           Tsh. 40,000/= kwa ajili ya kuwalipa wapishi, Walinzi na Matron
(vi)          Tsh.   2,000/= Nembo ya shule
(vii)         Tsh. 10,000/= kwa ajili ya huduma ya kwanza
(viii)       Tsh. 20,000/= Mitihani ya kujipima
(ix)          Tsh.   5,000/= Tahadhari (Haitarejeshwa)
 JUMLA YA MICHANGO YOTE NI TSH.  123,000/=.
  Fedha hiyo ilipwe katika akaunti ya Shule Na. 30201200045 iitwayo NATTA SECONDARY SCHOOL katika Benki ya NMB Tawi lolote na alete Bank Pay in Slip Original Shuleni iliyoandikwa Jina sahihi la Mwanafunzi.

2.2.  Sare ya Darasani:
  (i)   Sketi mbili (2) rangi ya Dark Bluu zilizoshonwa vizuri mshono wa rinda box    
        Lenye marinda mawili pembeni na urefu wake ufike kwenye kisigino.
 (ii)  Shati (blouse) mbili (2) nyeupe za mikono mirefu na isiyobana mwilini.
(III)  Viatu vyeusi vya ngozi vya kufunga kwa kamba vyenye visigino vifupi jozi 2
(iv)  Sweta zito  rangi ya dark bluu lenye shingo ya V.
 (v)  Wanafunzi wa kiislamu wataruhusiwa kushona hijabu inayofanana na sare ya
       shule (Iwe ya rangi nyeupe) jozi mbili (2).
(vi) Soksi nyeupe ndefu jozi mbili (2)
N.B: Wanafunzi hawaruhusiwi kusuka nywele; kuweka dawa kichwani; kutumia
        Vipodozi au kuja nguo nyingi za nyumbani

2.3: Vifaa vya Darasani.
      (i) Dafatari QUIRE 3(3Q) zisizopungua 7 na kubwa 9 kwa ajili ya majaribio     
      (ii) Kalamu  na penseli     (iii)    Rimu moja (1) ya karatasi (double A)
      (iii) Mathematical set (Bofa) kwa wanaochukua Jografia.
      (iv)  Kikokotozi (Calculator) kwa wanaochukua Jiografia  
      (v) Vitabu vya masomo ya tahasusi (mchepuo) utakaochukua visivyopungua viwili.
MUHIMU: VITABU HIVI VITAKAGULIWA SIKU YA KURIPOTI SHULENI KATIKA OFISI YA TAALUMA.

2.4.  Mahitaji mengine anayopaswa kuja nayo mwanafunzi
·       Sanduku la chuma la kutunzia vifaa vyake binafsi na kufuri imara
·       Njoo na Godoro la futi 2.5 X 6
·       Njoo na Tsh. 20,000/= kwa ajili ya T-Shirt 2 zenye Nembo ya Shule
·       Njoo na Barakoa au Tsh 2000/= kwa ajili ya kushona Barakoa mbili (2) shuleni
·       Shuka mbili rangi ya pink na moja rangi nyeupe isiyokuwa na maua; Blanket rangi yoyote; Mto (Foronya) rangi ya Pink;  Taulo
·       Galon ya Lt 5 ya kuhifadhia maji ya kunywa;
·       Net ya mbu Futi 4×6 (Rangi Nyeupe)
·       Mshonee mwanao gauni la kushindia (shamba dress) rangi ya kijivu. Trucksuit rangi ya Nyekundu au Dark Blue isiyobana mwili na nzito kwa ajili ya mchakamchaka,
·       Fedha ya matumizi binafsi ya mwanafunzi isiyopungua Tsh 40,000/= itakayotunzwa na Matron/ Patron;
·       Toilet tissue za kutosheleza matumizi yake (Zinapatikana )
·       Pedi za kutosha (Zinapatikana shuleni)
·       Kiwi nyeusi na Brush yake. Vifaa vya usafi Tsh. 10,000/= aje nazo shuleni.
·       Tochi aina ya D.Light moja kwa matumizi wakati umeme unapokatika
·       Nyuzi za kuogea
·       Marapa/kandambili za kwendea bafuni
·       Kanga/kitenge jozi moja
·       Kioo cha kujitazamia usoni; Saa ya kuvaa mkononi
·       Mafuta ya kujipaka mwilini; Sabuni; Miswaki na dawa ya meno;
2.5. Huduma ya chakula shuleni.
          Mwanao atatakiwa kuja na vifaa vya chakula (Sahani;  Kikombe; Kijiko).

2.6.  Malipo ya matibabu na nauli.
-  Jukumu la matibabu ni la mzazi/mlezi wa mwanafunzi. Shule itahusika na huduma ya kwanza tu. Endapo ana magonjwa ya kudumu mfano Pumu (Asthma) anashauriwa kuja na dawa anazotumia au Bima ya Afya kama anayo
            -   Nauli ya kuja shuleni na kurudi nyumbani wakati wa likizo ni jukumu la
            mzazi/mlezi wa mwanafunzi
  
3.0:  Sheria  na kanuni za shule.
Shule inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na kama ilivyorekebishwa kwa sheria Na. 10 ya mwaka 1995. Aidha inazingatia miongozo yote inayotolewa na wizara yenye dhamana ya Elimu; Sayansina Teknolojia Nchini chini ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI yenye jukumu la Usimamizi na Uendeshaji Elimu. Unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo ambayo yatafafanuliwa kwa maandishi  na utapewa mara baada ya kuripoti shuleni.
(a)  Hashima kwa watu wote (viongozi wa serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa na wale wa serikali ya wanafunzi ; wazazi, walimu, wanafunzi wengine)
(b)   Mahudhurio mazuri katika shughuli za ndani na nje  ya shule kulingana na ratiba ya shule ni lazima.
(c)  Kushiriki kwa makini kufanya maandalio ya jioni (preparation).
(d)  Kuwahi katika kila shughuli za shule na nyingine zitakazotolewa.
(e)  Kufahamu mipaka ya shule na kuzingatia kikamilifu maelekezo juu ya kuwepo ndani  na nje ya mipaka hiyo wakati wote wa uanafunzi wako katika shule hii.
(f)    Kutunza usafi wa mwili, mavazi, na mazingira ya shule.
(g)  Kuvaa sare ya shule wakati wote unapotakiwa.
(h)  Kuzingatia ratiba ya shule wakati wote.
(i)     (i)Kutunza mali za umma.

3.1:  Makosa yafuatayo yanaweza kusababisha ukafukuzwa au kusimamishwa
        shule:
       (i)   Wizi wa mali ya shule na wanafunzi wengine.
       (ii)  Kujihusisha na ngono, uasherati, ushoga, ulawiti, usagaji na ubakaji.
      (iii)   Ulevi wa pombe na kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya
       (iv)  Kupiga, kupigana au kuchochea ugomvi.
      (v)   Kuharibu mali ya umma kwa makusudi na kukataa kulipa fidia ya uharibifu  
      (Vi)  Kakataa kupokea adhabu halali na kuonyesha kiburi, dharau na ufedhuri,    
      (vii)  Kumiliki; kukutwa au kutumia simu ya mkononi katika mazingira ya shule
      (viii)  Kuolewa, kupatikana na ujazito, kutoa mimba au kushawishi kutoa mimba.
       (ix)  Kushiriki au kushawishi kugoma, kuchochea au kuvuruga amani na 
                usalama wa shule na watu wengine.
        (x)  Kudharau bendera ya Taifa, viongozi wa serikali, vyama vya siasa,
               madhehebu ya dini, shule.
       (xi)  Utoro wa muda mrefu, kushindwa kufanya kazi za darasani na nje,
      (Xii)  Kushindwa kufanya mazoezi/majaribio /mitihani pamoja na kutohudhuria 
               maandalizi ya usiku (Night Preparation).
     (xiii)  Kutoa lugha ya matusi kwa walimu; wafanyakazi wasio walimu au viranja   
               wa shule.
   (xiv)  Kulala nje ya shule; kutembelea majumba ya starehe na nyumba za wageni
   (xv)   Kutumia vifaa vya umeme kama vile Heater; radio; pasi ya umeme
  (xvi)  Kutembelea nyumba za walimu/watumishi wa shule bila ya kufuata taratibu
                za  shule
   (xvi)  Kujipikia/kuingiza vyakula bwenini
   (xvii)  Kukutwa nje ya shule bila ruhusa na mavazi yasiyoruhusiwa shuleni
  (xviii)  Kudharau Bendera ya Taifa; Wimbo wa Taifa au Viongozi wa Nchi.
  (xvix)  Kufanya jaribio lolote la kujiua, kutishia kujiua kama kunywa sumu n.k
    (xx)   Kusuka nywele kwa mtindo usiokubalika au kunyoa mtindo wa kihuni.

4.0: Mambo mengine Muhimu yanayopaswa kukamilishwa na kuwasilishwa
       shuleni na mwanafunzi:
            (a)  Fomu ya Hospitali (Medical Examination Form) ambayo itajazwa na   
                  Mganga Mkuu wa Hospitali a Serikali. Fomu hii itakabidhiwa  kwa Mkuu
                  wa Shule mara atakaporipoti shuleni.
            (b)  Fomu ya Maelezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi na mkataba wa
                   kutoshiriki  katika migomo, fujo, na makosa ya jinai.
            (c)  Fomu ya mzazi kukiri kukubaliana na sheria, kanuni, na maelekezo
                  Mengine yatakayotolewa na shule.Barua/Fomu ya kukuita shulenI

5.0: Hitimisho Muhimu: Tafadhali soma kwa makini maelezo haya na kuyatekeleza    
                                         kikamilifu.     
1.    Hutupokei Fedha Taslimu Shuleni. Hivyo malipo yote yapitie BENKIISIPOKUWA malipo ya vifaa vinavyoweza kupatikana shuleni.
2.    Mwanao haruhusiwi kuja shuleni na simu ya kiganjani, pasi ya umeme,redio, heater, computer na TV. AKIPATIKANA NA VIFAA HIVI ADHABU NI KUONDOLEWA SHULENI AU KUTOZWA FIDIA YA UHARIBIFU.
3.    Haturuhusu mwananunzi kutembelewa shuleni na watu wasiofahamika.
4.    Mwanafunzi anatakiwa kuwahi bwaloni mara kengele ya chakula inapogonga akiwa na vyombo vya chakula
5.    Shule haina utaratibu wa kutoa chakula maalum (special diet) kwa wale wenye matatizo ya kiafya ya kutokula baadhi ya vyakula
6.    Mwanafunzi atumiwe nauli mapema kabla ya kufunga shule ili utaratibu wa usafiri uweze kuandaliwa mapema.
7.    Ratiba ya shule huanza saa 11:30 Alfajiri kwa mchakamchaka; kufanya usafi binafsi na wa mazingira ya bwenini.
8.    Mwanafunzi ataruhusiwa kusali katika dhehebu lake shuleni kulingana na utaratibu uliowekwa na shule
9.    Masiliano ya mwanafunzi na mzazi/mlezi yapitie katika uongozi wa shule..
Hakikisha mwanao anakuja na mahitaji yote muhimu na anaripoti kwa wakati akiwa na.
v  Barua/Fomu hii ya kujiunga shuleni
v  Bank pay in Slips original ya malipo yalipitia benki
v  Nakala ya ‘Result Slip inayoonesha matokeo ya kidato cha IV
v  Nakala ya cheti cha kuzaliwa kama anacho
v  Fedha ya kulipia mahitaji yanayopatikana shuleni kama ilivyoelekezwa kwenye fomu hii
v  Vifaa/mahitaji yote muhimu kwa matumizi binafsi/shule
v  Fomu ya Hospitali; na ya Maelezo binafsi zijazwe kwa usahi
SCHOOL MOTTO: “STRIVE FOR EXCELLENCY”
KARIBU SANA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NATTA
...........................
MOHAMED B. KAJERI
MKUU WA SHULE


SHULE YA SEKONDARI NATTA
FOMU YA KUTHIBITISHA AFYA YA MWANAFUNZI
(Ijazwe na Mganga wa Hospitali ya Serikali au Kituo cha Afya cha Serikali tu)
Kumb. Na. KSS/MEDICAL/ F.V                                           Tarehe ......../........../2020

Mganga Hospitali / Kituo cha Afya.....................................................
S.L.P....................
......................................

YAH: KUPIMWA HALI YA AFYA YA MWANAFUNZI..................................................
Shule ya Sekondari Kasoma inakuomba kumpima na kujaza taarifa ya Afya ya mwanafunzi mtajwa hapo juu kabla ya kujiunga na masomo ya sekondari.
       i Macho (Vision)............................................................................................................
ii Kifua kikuu(TB)............................................................................................................
iii Pumu (Asthma)..........................................................................................................
ivShinikizo la Damu (Blood Pressure)..........................................................................
v Kisukari (Diabetes).....................................................................................................
vi Magonjwa ya zinaa (Veneral Diseases)....................................................................
vii Matatizo ya Usikivu (Hearing)..................................................................................
viii Malaria sugu.............................................................................................................
ix Ulemavu wa viungo (Physical disability). Taja............................................................
x Mimba kwa msichana (Pregnancy)......................................................................
xi Matatizo akili (Mental disability)..........................................................................
xii Matatizo ya moyo (Heart problems)...................................................................
xiii Matatizo ya tumbo(Abdomen)...........................................................................
xiv Damu(Bllod examination)...................................................................................
xv Kusumbuliwa na kichwa(Headache)..................................................................
xvi Kichocho ( bilharziasis)......................................................................................
xiii Maradhi mengine (Other infections if any).......................................................
.................................................................................................................................

Note: In case of any health problem detected; it is recommended that a student should get treatment before coming to school.

I have examined the above student and declare that he/she is physically and mentally fit for joining advanced level studies.

Name & Signature of the examiner:....................................................
    
Desighation.........................................Station...............................   Date...........................
OFFICIAL RUBBERSTAMP


FOMU YA KUKIRI KUKUBALIANA NA TARATIBU ZA SHULE .
SEHEMU YA I: IJAZWE NA MWANAFUNZI MWENYEWE
Mimi.....................................................................................nimezisoma sheria; kanuni na taratibu za shule na kuzielewa vizuri bila ya shaka yoyote. Ninaahidi kuzitii na kutozivunja katika kipindi changu chote cha kusoma kwangu katika shule ya Natta sekondari. Vilevile, nitajitahidi kusoma kwa bidii na kushiriki shughuli zote za nje kulingana na ratiba ya shule. Endapo nitakwenda kinyume na kiapo cha ahadi yangu, basi uongozi wa shule unichukulie hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kupewa adhabu kali/kusimamishwa masomona hata kufukuzwa shule.
Dini................................ Dhehebu....................... Tarehe ya kuzaliwa.............................
Michezo uipendayo/Hobbies.............................................................................................
Kazi ya mzazi/mlezi................................................... mahali.............................................
Wilaya.................................... Mkoa............................... Simu...........................................
     Jinala mwanafunzi............................................... Saini.....................Tarehe........,,,,,,.......

SEHEMU YA II: IJAZWE NA MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI.
Mimi...............................................................ambaye ni mzazi/mlezi wa mwanafunzi........
....................................................kidato cha Tano mwaka 2020/21;
Ninakiri kuwa nimeyasoma maelekezo ya kujiunga na shule ya sekondari Natta nikiwa na mwanangu na kuyaelewa vizuri. Ninaahidi kushirikiana na uongozi wa shule katika kuhakikisha kuwa mwanangu anazingatia taratibu zote hizo wakati wa kipindi cha masomo yake. Pia, nitampatia mahitaji yake yote muhimu ya shule ikiwa ni pamoja na malipo; mahitaji binafsi na kufuatilia mwenendo wake kitaaluma na nidhamu na niko tayari kupokea maamuzuzi yoyote yatakotolewa na uongozi wa shule endapo mwanangu atavunja taratibu; kanuni; na sheria za shule.
Mwisho, endapo nitashindwa kutimiza jukumu langu la kumlipia mwanangu ada na michango halali ya shule kwa wakati, niko tayari kuwajibishwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya kisheria kwani kufanya hivyo ni kuzorotesha maendeleo ya mwanangu na mipango ya shule kwa ujumla.
Jina la mzazi...................................................Saini............................Tarehe....................
SEHEMU YA III: UHUSIANO WA MWANAFUNZI NA NDUGU/JAMAA WENGINE.
Tafadhali jaza majina; namba za simu na kuonyesha uhusiano  uliopo kati  ya ndugu/jamaa  wa mwanafunzi kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano na uongozi wa shule.
NA
JINA LA NDUGU
UHUSIANO
NA. SIMU
ANAKOISHI
KAZI





















ASANTE KWA USHIRIKIANO WAKO

Click here to Download Joining Instruction


MWONEKANO WA SARE ZA SHULE

MWONEKANO WA GAUNI LA KUSHINDIA (SHAMBA DRESS)

MWONEKANO WA SKETI YA KUSHINDIA-UREFU HADI KWENYE VIFUNDO VYA MIGUU

MWONEKANO WA SKETI YA DARASANI-UREFU HADI KWENYE VIFUNDO VYA MIGUU


KARIBUNI NATTA SEKONDARI