Click here 👇 to Download Joining Instruction
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS – TAMISEMI
SHULE YA SEKONDARI NATTA, S.L.P 192, MUGUMU-SERENGETI
Namba za
Simu:
Mkuu wa Shule:
0752- 985030 au 0787- 985030
M/Mkuu wa shule:0753 – 741530
Mwandamizi taaluma: 0686 - 777374
Mtatron: 0755 - 057448
Tarehe: 30 /05/2020
************************************************************************************************
Mzazi/Mlezi wa Mwanafunzi........................................................S.L.P..........
YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA
SEKONDARI NATTA; HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI
MKOA WA MARA MWAKA 2020.
Utangulizi:
Ninafurahi kukutaarifu kuwa
mwanao------------------------------------------amechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano
tahasusi ya..................... katika shule ya sekondari ya NATTA. Muhula wa
masomo utaanza……………. Hivyo mwanao anatakiwa kuripoti shuleni tarehe……………… kwa
usajili na masomo yataanza rasmi tarehe ………. Mwisho wa kuripoti ni tarehe ………………….
Mahali
shule ilipo
Shule ya sekondari ya Natta ipo Mkoa wa Mara; Wilaya ya
Serengeti; Tarafa ya Grumeti; Kata ya Natta umbali wa kilometa arobaini (40)
kutoka makao makuu ya wilaya (Mugumu). Usafiri wa barabara ni wa uhakika muda
wote.
Jinsi
ya kufika Shuleni
(i)
Wanaotoka Dar-Es-Salaam, Pwani; Morogoro; Mikoa
ya Kati; Kusini; Nyanda za juu kusini; Kigoma; Kagera baada ya kufika Mwanza
wanashauriwa kupanda Mabasi Stendi ya Buzuruga-Mwanza yanayokuja Mugumu kupitia
Bunda. Nauli kutoka Mwanza ni kati ya Tsh. 15,000/= hadi 20,000/=.
(ii)
Kwa wale wanaotokea Mikoa ya Kaskazini
(Kilimanjaro; Arusha; Manyara na Tanga) wapande mabasi yanayokwenda Musoma
kupitia barabara ya Ngorongoro-Serengeti. Nauli kutoka arusha mjini ni Tsh.
45,000/=
(iii)
Kwa wanaotoka Mkoa wa Mara wanaweza kupandia
stendi kuu za mabasi yatokayo Musoma, Bunda; au Tarime kuja Mugumu Kupitia
Butiama; Nyamswa; Isenye na Kushukia Natta Sekondari. Nauli ni ati ya Tsh.
10,000/= hadi 15,000/= kufika shuleni.
*
Mwanafunzi anashauriwa kumuomba mhudumu wa gari (Dereva au Condactor)
alilopanda kumshushia KIBAO CHA SHULE YA SEKONDARI NATTA.
2.0.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.
2.1
Ada na Michango ya Shule:
(a) Ada ya shule kwa mwaka ni Tsh. 70,000/=. Unaweza kulipa Tsh. 35,000/=
kwa muhula au kulipa ada yote kwa mara moja.
Fedha hiyo ya ada ilipwe kenye Akaunti
ya Shule Na. 30201200045
ilitwayo NATTA SECONDARY SCHOOL katika
Benki ya NMB Tawi lolote
na lete Bank Pay in Slip Original
shuleni iliyoandikwa Jina sahihi la
Mwanafunzi.
(b)
Michango inayotakiwa kulipwa na kila mzazi ni:-
(i) Tsh. 20,000/= kwa ajili ya ukarabati wa samani
(ii) Tsh. 6,000/= kwa ajili ya kitambulisho na picha
(iv)
Tsh. 20,000/=
kwa ajili ya taaluma
(v)
Tsh. 40,000/=
kwa ajili ya kuwalipa wapishi, Walinzi na Matron
(vi)
Tsh. 2,000/= Nembo ya shule
(vii)
Tsh. 10,000/=
kwa ajili ya huduma ya kwanza
(viii) Tsh. 20,000/= Mitihani ya kujipima
(ix)
Tsh. 5,000/= Tahadhari (Haitarejeshwa)
JUMLA YA MICHANGO YOTE NI TSH. 123,000/=.
Fedha
hiyo ilipwe katika akaunti ya Shule Na. 30201200045
iitwayo NATTA SECONDARY SCHOOL katika Benki ya NMB Tawi lolote na alete Bank Pay in Slip Original Shuleni
iliyoandikwa Jina sahihi la Mwanafunzi.
2.2.
Sare ya
Darasani:
(i) Sketi mbili (2) rangi ya Dark
Bluu zilizoshonwa vizuri mshono wa rinda
box
Lenye marinda mawili pembeni na urefu
wake ufike kwenye kisigino.
(ii) Shati (blouse) mbili (2) nyeupe za mikono
mirefu na isiyobana mwilini.
(III) Viatu vyeusi vya ngozi vya
kufunga kwa kamba vyenye visigino vifupi jozi 2
(iv) Sweta zito rangi ya dark bluu lenye shingo ya V.
(v) Wanafunzi
wa kiislamu wataruhusiwa kushona hijabu inayofanana na sare ya
shule (Iwe ya rangi nyeupe) jozi mbili (2).
(vi) Soksi nyeupe ndefu jozi mbili (2)
N.B: Wanafunzi hawaruhusiwi kusuka nywele; kuweka
dawa kichwani; kutumia
Vipodozi au kuja nguo nyingi za nyumbani
2.3:
Vifaa vya Darasani.
(i)
Dafatari QUIRE 3(3Q) zisizopungua 7 na kubwa 9 kwa ajili ya majaribio
(ii) Kalamu na penseli (iii)
Rimu
moja (1) ya karatasi (double A)
(iii) Mathematical set (Bofa) kwa wanaochukua Jografia.
(iv) Kikokotozi (Calculator) kwa wanaochukua
Jiografia
(v)
Vitabu vya masomo ya tahasusi (mchepuo)
utakaochukua visivyopungua viwili.
MUHIMU:
VITABU HIVI VITAKAGULIWA SIKU YA KURIPOTI SHULENI KATIKA OFISI YA TAALUMA.
2.4. Mahitaji
mengine anayopaswa kuja nayo mwanafunzi
· Sanduku
la chuma la kutunzia vifaa vyake binafsi na kufuri imara
·
Njoo na Godoro la futi 2.5 X 6
·
Njoo na Tsh. 20,000/= kwa ajili ya T-Shirt 2
zenye Nembo ya Shule
·
Njoo
na Barakoa au Tsh 2000/= kwa ajili ya kushona Barakoa mbili (2) shuleni
·
Shuka mbili rangi ya pink na moja rangi nyeupe isiyokuwa na maua;
Blanket rangi yoyote; Mto (Foronya) rangi ya Pink; Taulo
·
Galon ya Lt 5 ya kuhifadhia maji ya kunywa;
·
Net ya mbu Futi 4×6 (Rangi Nyeupe)
·
Mshonee
mwanao gauni la kushindia (shamba dress) rangi ya kijivu. Trucksuit rangi ya Nyekundu au Dark Blue isiyobana mwili
na nzito kwa ajili ya mchakamchaka,
·
Fedha ya matumizi binafsi ya mwanafunzi
isiyopungua Tsh 40,000/= itakayotunzwa na Matron/ Patron;
·
Toilet tissue za kutosheleza matumizi yake
(Zinapatikana )
·
Pedi za kutosha (Zinapatikana shuleni)
·
Kiwi nyeusi na Brush yake. Vifaa vya usafi Tsh.
10,000/= aje nazo shuleni.
·
Tochi aina ya D.Light moja kwa matumizi wakati
umeme unapokatika
·
Nyuzi za kuogea
·
Marapa/kandambili za kwendea bafuni
·
Kanga/kitenge jozi moja
·
Kioo cha kujitazamia usoni; Saa ya kuvaa
mkononi
·
Mafuta ya kujipaka mwilini; Sabuni; Miswaki na
dawa ya meno;
2.5. Huduma
ya chakula shuleni.
Mwanao atatakiwa kuja na vifaa vya chakula (Sahani; Kikombe; Kijiko).
2.6. Malipo ya matibabu na nauli.
- Jukumu
la matibabu ni la mzazi/mlezi wa mwanafunzi. Shule itahusika na huduma ya
kwanza tu. Endapo ana magonjwa ya kudumu mfano Pumu (Asthma) anashauriwa kuja
na dawa anazotumia au Bima ya Afya kama anayo
- Nauli ya kuja shuleni na
kurudi nyumbani wakati wa likizo ni jukumu la
mzazi/mlezi wa mwanafunzi
3.0: Sheria
na kanuni za shule.
Shule
inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na kama
ilivyorekebishwa kwa sheria Na. 10 ya mwaka 1995. Aidha inazingatia miongozo
yote inayotolewa na wizara yenye dhamana ya Elimu; Sayansina Teknolojia Nchini
chini ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI yenye jukumu la Usimamizi na Uendeshaji Elimu.
Unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo ambayo yatafafanuliwa kwa
maandishi na utapewa mara baada ya
kuripoti shuleni.
(a) Hashima kwa watu wote (viongozi wa serikali,
madhehebu ya dini, vyama vya siasa na wale wa serikali ya wanafunzi ; wazazi,
walimu, wanafunzi wengine)
(b) Mahudhurio mazuri katika shughuli za ndani na
nje ya shule kulingana na ratiba ya
shule ni lazima.
(c) Kushiriki kwa makini kufanya maandalio ya jioni
(preparation).
(d) Kuwahi katika kila shughuli za shule na nyingine
zitakazotolewa.
(e) Kufahamu mipaka ya shule na kuzingatia
kikamilifu maelekezo juu ya kuwepo ndani
na nje ya mipaka hiyo wakati wote wa uanafunzi wako katika shule hii.
(f) Kutunza usafi wa mwili, mavazi, na mazingira ya
shule.
(g) Kuvaa sare ya shule wakati wote unapotakiwa.
(h) Kuzingatia ratiba ya shule wakati wote.
(i) (i)Kutunza mali za umma.
3.1: Makosa yafuatayo yanaweza kusababisha
ukafukuzwa au kusimamishwa
shule:
(i) Wizi wa mali ya shule na
wanafunzi wengine.
(ii) Kujihusisha na ngono,
uasherati, ushoga, ulawiti, usagaji na ubakaji.
(iii) Ulevi wa pombe na
kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya
(iv) Kupiga, kupigana au
kuchochea ugomvi.
(v) Kuharibu mali ya umma kwa
makusudi na kukataa kulipa fidia ya uharibifu
(Vi) Kakataa kupokea adhabu
halali na kuonyesha kiburi, dharau na ufedhuri,
(vii) Kumiliki; kukutwa au
kutumia simu ya mkononi katika mazingira ya shule
(viii) Kuolewa, kupatikana na
ujazito, kutoa mimba au kushawishi kutoa mimba.
(ix) Kushiriki au kushawishi
kugoma, kuchochea au kuvuruga amani na
usalama wa shule na watu wengine.
(x) Kudharau bendera ya Taifa,
viongozi wa serikali, vyama vya siasa,
madhehebu ya dini, shule.
(xi) Utoro wa muda mrefu,
kushindwa kufanya kazi za darasani na nje,
(Xii) Kushindwa kufanya
mazoezi/majaribio /mitihani pamoja na kutohudhuria
maandalizi ya usiku (Night Preparation).
(xiii) Kutoa lugha ya matusi kwa
walimu; wafanyakazi wasio walimu au viranja
wa shule.
(xiv) Kulala nje ya shule;
kutembelea majumba ya starehe na nyumba za wageni
(xv) Kutumia vifaa vya umeme
kama vile Heater; radio; pasi ya umeme
(xvi) Kutembelea nyumba za
walimu/watumishi wa shule bila ya kufuata taratibu
za shule
(xvi) Kujipikia/kuingiza vyakula
bwenini
(xvii) Kukutwa nje ya shule bila
ruhusa na mavazi yasiyoruhusiwa shuleni
(xviii) Kudharau Bendera ya
Taifa; Wimbo wa Taifa au Viongozi wa Nchi.
(xvix) Kufanya jaribio lolote la
kujiua, kutishia kujiua kama kunywa sumu n.k
(xx) Kusuka nywele kwa mtindo
usiokubalika au kunyoa mtindo wa kihuni.
4.0:
Mambo mengine Muhimu yanayopaswa kukamilishwa na kuwasilishwa
shuleni na mwanafunzi:
(a)
Fomu ya Hospitali (Medical Examination Form) ambayo itajazwa na
Mganga Mkuu wa Hospitali a
Serikali. Fomu hii itakabidhiwa kwa Mkuu
wa Shule mara atakaporipoti
shuleni.
(b)
Fomu ya Maelezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi na mkataba wa
kutoshiriki katika migomo, fujo, na makosa ya jinai.
(c)
Fomu ya mzazi kukiri kukubaliana na sheria, kanuni, na maelekezo
Mengine yatakayotolewa na
shule.Barua/Fomu ya kukuita shulenI
5.0:
Hitimisho Muhimu: Tafadhali soma
kwa makini maelezo haya na kuyatekeleza
kikamilifu.
1. Hutupokei Fedha Taslimu Shuleni. Hivyo malipo
yote yapitie BENKIISIPOKUWA malipo ya vifaa
vinavyoweza kupatikana shuleni.
2. Mwanao haruhusiwi kuja shuleni na simu ya
kiganjani, pasi ya umeme,redio, heater, computer na TV. AKIPATIKANA NA VIFAA
HIVI ADHABU NI KUONDOLEWA SHULENI AU KUTOZWA FIDIA YA UHARIBIFU.
3. Haturuhusu mwananunzi kutembelewa shuleni na
watu wasiofahamika.
4. Mwanafunzi anatakiwa kuwahi bwaloni mara
kengele ya chakula inapogonga akiwa na vyombo vya chakula
5. Shule haina utaratibu wa kutoa chakula maalum
(special diet) kwa wale wenye matatizo ya kiafya ya kutokula baadhi ya vyakula
6. Mwanafunzi atumiwe nauli mapema kabla ya
kufunga shule ili utaratibu wa usafiri uweze kuandaliwa mapema.
7. Ratiba ya shule huanza saa 11:30 Alfajiri kwa
mchakamchaka; kufanya usafi binafsi na wa mazingira ya bwenini.
8. Mwanafunzi ataruhusiwa kusali katika dhehebu
lake shuleni kulingana na utaratibu uliowekwa na shule
9. Masiliano ya mwanafunzi na mzazi/mlezi yapitie
katika uongozi wa shule..
Hakikisha mwanao anakuja na mahitaji yote
muhimu na anaripoti kwa wakati akiwa na.
v Barua/Fomu hii ya kujiunga shuleni
v Bank pay in Slips original ya malipo yalipitia
benki
v Nakala ya ‘Result Slip inayoonesha matokeo ya
kidato cha IV
v Nakala ya cheti cha kuzaliwa kama anacho
v Fedha ya kulipia mahitaji yanayopatikana
shuleni kama ilivyoelekezwa kwenye fomu hii
v Vifaa/mahitaji yote muhimu kwa matumizi
binafsi/shule
v Fomu ya Hospitali; na ya Maelezo binafsi
zijazwe kwa usahi
SCHOOL MOTTO: “STRIVE FOR EXCELLENCY”
KARIBU SANA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NATTA
...........................
MOHAMED B. KAJERI
MKUU WA SHULE
SHULE YA SEKONDARI NATTA
FOMU YA KUTHIBITISHA AFYA YA MWANAFUNZI
(Ijazwe na Mganga wa Hospitali ya Serikali au
Kituo cha Afya cha Serikali tu)
Kumb.
Na. KSS/MEDICAL/ F.V
Tarehe ......../........../2020
Mganga
Hospitali / Kituo cha Afya.....................................................
S.L.P....................
......................................
YAH:
KUPIMWA HALI YA AFYA YA
MWANAFUNZI..................................................
Shule ya Sekondari Kasoma inakuomba kumpima na kujaza taarifa ya Afya
ya mwanafunzi mtajwa hapo juu kabla ya kujiunga na masomo ya sekondari.
i
Macho
(Vision)............................................................................................................
ii Kifua kikuu(TB)............................................................................................................
iii Pumu
(Asthma)..........................................................................................................
ivShinikizo la Damu (Blood Pressure)..........................................................................
v Kisukari
(Diabetes).....................................................................................................
vi Magonjwa ya zinaa (Veneral
Diseases)....................................................................
vii Matatizo ya Usikivu
(Hearing)..................................................................................
viii Malaria
sugu.............................................................................................................
ix Ulemavu wa viungo (Physical disability).
Taja............................................................
x Mimba kwa msichana
(Pregnancy)......................................................................
xi Matatizo akili (Mental
disability)..........................................................................
xii Matatizo ya moyo (Heart
problems)...................................................................
xiii Matatizo ya tumbo(Abdomen)...........................................................................
xiv Damu(Bllod
examination)...................................................................................
xv Kusumbuliwa na
kichwa(Headache)..................................................................
xvi Kichocho (
bilharziasis)......................................................................................
xiii Maradhi mengine (Other infections if
any).......................................................
.................................................................................................................................
Note: In case of any health problem detected;
it is recommended that a student should get treatment before coming to school.
I have examined the above student and declare
that he/she is physically and mentally fit for joining advanced level studies.
Name & Signature of the
examiner:....................................................
Desighation.........................................Station............................... Date...........................
OFFICIAL RUBBERSTAMP
FOMU
YA KUKIRI KUKUBALIANA NA TARATIBU ZA SHULE .
SEHEMU YA
I: IJAZWE NA MWANAFUNZI MWENYEWE
Mimi.....................................................................................nimezisoma sheria; kanuni na taratibu za shule na
kuzielewa vizuri bila ya shaka yoyote. Ninaahidi kuzitii na kutozivunja katika kipindi changu chote cha kusoma
kwangu katika shule ya Natta sekondari. Vilevile, nitajitahidi kusoma kwa bidii
na kushiriki shughuli zote za nje kulingana na ratiba ya shule. Endapo
nitakwenda kinyume na kiapo cha ahadi yangu, basi uongozi wa shule unichukulie
hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kupewa
adhabu kali/kusimamishwa masomona hata kufukuzwa shule.
Dini................................
Dhehebu....................... Tarehe ya kuzaliwa.............................
Michezo
uipendayo/Hobbies.............................................................................................
Kazi ya
mzazi/mlezi...................................................
mahali.............................................
Wilaya....................................
Mkoa............................... Simu...........................................
Jinala
mwanafunzi...............................................
Saini.....................Tarehe........,,,,,,.......
SEHEMU YA
II: IJAZWE NA MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI.
Mimi...............................................................ambaye
ni mzazi/mlezi wa mwanafunzi........
....................................................kidato
cha Tano mwaka 2020/21;
Ninakiri
kuwa nimeyasoma maelekezo ya kujiunga na shule ya sekondari Natta nikiwa na
mwanangu na kuyaelewa vizuri. Ninaahidi kushirikiana na
uongozi wa shule katika kuhakikisha kuwa mwanangu anazingatia taratibu zote
hizo wakati wa kipindi cha masomo yake. Pia, nitampatia mahitaji
yake yote muhimu ya shule ikiwa ni pamoja na malipo; mahitaji binafsi na
kufuatilia mwenendo wake kitaaluma na nidhamu na niko tayari
kupokea maamuzuzi yoyote yatakotolewa na uongozi wa shule endapo mwanangu
atavunja taratibu; kanuni; na sheria za shule.
Mwisho,
endapo nitashindwa kutimiza jukumu langu la kumlipia mwanangu ada na michango
halali ya shule kwa wakati, niko tayari kuwajibishwa ikiwa ni pamoja na
kufikishwa katika vyombo vya kisheria kwani kufanya hivyo ni kuzorotesha
maendeleo ya mwanangu na mipango ya shule kwa ujumla.
Jina la mzazi...................................................Saini............................Tarehe....................
SEHEMU YA III: UHUSIANO WA MWANAFUNZI NA
NDUGU/JAMAA WENGINE.
Tafadhali jaza majina; namba za simu na
kuonyesha uhusiano uliopo kati ya ndugu/jamaa wa mwanafunzi kwa ajili ya kurahisisha
mawasiliano na uongozi wa shule.
NA
|
JINA LA
NDUGU
|
UHUSIANO
|
NA.
SIMU
|
ANAKOISHI
|
KAZI
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
ASANTE KWA USHIRIKIANO WAKO
Click here to Download Joining Instruction
MWONEKANO WA SARE ZA SHULE
MWONEKANO WA GAUNI LA KUSHINDIA (SHAMBA DRESS) |
MWONEKANO WA SKETI YA KUSHINDIA-UREFU HADI KWENYE VIFUNDO VYA MIGUU |
MWONEKANO WA SKETI YA DARASANI-UREFU HADI KWENYE VIFUNDO VYA MIGUUKARIBUNI NATTA SEKONDARI |
Ndugu wazazi/walezi
ReplyDeleteKwa niaba ya uongozi wa shule ya sekondari Natta, napenda kuwakaribisha sana mnapokuwa mkiwaleta wanafunzi shuleni. Katika ukurasa huu wa blogi ya shule tumeweka fomu ya kujiunga (Joining instruction) ambayo unaweza kuipakua (download) na ukaiprinti mahala popote ulipo na kukamilisha mahitaji ya mwanao. Hauna haja ya kusafiri umbali mrefu kuja shuleni kuchukua fomu hii.
Upatapo changamoto katika kuipakua fomu hii au masuala yahusuyo mfumo wetu tafadhali wasiliana nami kwa namba: 0715103790/0762177350; Jina ni Mwema M. Warioba.
Ahsanteni na karibuni Natta sekondari.
Ahsante kwa blog hii ya shule . Je Kuna mabadiriko yoyote Kati ya mwaka 2020 na 2021 katika join instruction?? Msaada tafadhari
ReplyDeleteSega TFT | Titanium Art | iTanium.com
ReplyDeleteTFT (also known as TFTs) is ford edge titanium 2021 a series of TFTs produced by ridge titanium wallet Sega. The TFTs are similar pure titanium earrings to the Sega 2019 ford fusion hybrid titanium Mega Drive which have been used titanium knife by Sega.